Latest News

WASICHANA WATOANA JASHO AIRTEL RISING STARS



Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto) akichuana na mchezaji wa timu ya Simba Queens Mwanaidi Hamisi katika michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.

Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Simba Queens Asha Abdul katika michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.

Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Simba Queens Eva Charles (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Ilala Fatuma Salumu katika michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0

Timu ya wasichana ya Simba Queens jana iliibuka na ushindi wa 2 – 0 dhidi ya timu ya Ilala katika michuano ya vijana ya U-17 ya Airtel Rising Stars kwa mkoa wa kisoka wa Ilala. Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam jana.
Timu zilianza mchezo huo kwa kujihami na kushambuliana kwa kushtukiza. Simba Queens walifanikiwa kupata goli la mapema baada ya Zainab Mahmoud kuifungia timu yake katika dakika ya tano.
Timu ya Ilala ilibadilika baada ya kuwa nyuma kwa goli moja na kuanza kushambulia kwa kasi. Lakini juhuhudi hizo hazikuzaa matunda na hadi mapumziko timu ya Simba Queens walikua wanaongoza kwa goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikicheza kwa umakini wa hali ya juu. Simba Queens waliongeza kasi na kufanikiwa kupata goli la pili katika dakika ya 46 kupitia kwa Khadija Ally baada ya kuachia shuti kali lililotinga wavuni moja kwa moja.
Katika kiwanja cha Tanganyika Packers, Mburahati Queens iliichakaza Lulu Queens kwa magoli 2 -1. Wafungaji wa Mburahati Queens walikua ni Anne Adrea dakika ya 56 na Janeth Christopher dakika ya 90. Wakati kwa upande wa Lulu walipata goli lao kupitia kwaOpah Clement dakika ya 46.
Katika kiwanja cha Makangarawe Yombo Timu ya wavulana ya Wakati Ujao ilipata ushindi wa 2 -1 dhidi ya Dubu. Kwa upande wa wasichana timu za Evergreen Queens na Temeke Queens zilienda sare ya bila kufungana.
Michuano hii ya vijana ambayo kwa jiji la Dar es Salaam imeshaanza kwa takriban katika mikoa yake yote ya kimichezo, inafuatiliwa kwa karibu na jopo la makocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) bila kusahau timu mbalimbali ambazo zinawanyatia kwa karibu vijana wenye vipaji kutoka michuano hiyo.
Huu ni mwaka wa tano kwa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuanzisha na kudhamini michuano hiyo ya Airtel Rising Stars yenye lengo la kutafuta na kuendeleza vipaji.
Mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka huu yanajumuisha mikoa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha ambapo fainali za taifa za michezo hiyo zimepagwa kupigwa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21.


French Montana Ft Rick Ross & Lil Wayne ‘Lose It’ 


Coke Boys wamekuja pamoja na kutengenza video, ni French Montana kwenye video ya “Lose It,” akiwa na Rick Ross na Lil Wayne.


Video mpya ya Yo Gotti Ft Young Thug ‘Rihanna’ itazame hapa


Rapa Yo Gotti na Young Thug wamekuja pamoja kwa kishindo na kufanya wimbo.Angalia video>>>.Wimbo upo kwenye album yake mpya ya The Art of Hustle 
(Yo Gotti).

Post ya Ommy Dimpoz Instagram yazua uvumi.


Star wa bongo fleva kutoka Tanzania Ommy Dimpoz amepost picha ya mtoto mzuri kutoka Ethiopia anayeishi Marekani #WCE #QueenNBae‘. Binti huyu anaitwa Zerthun.

Zerthun

Timaya kwenye issue yake ya ubakaji inampa wakati mgumu.


Imekuwa furaha kubwa sana kwake Timaya baada ya kutangaza rasmi kwa kupata jina la mtoto wao wa kike. Mtoto huyu mwenye mwezi mmoja na siku chache amepewa jina Grace.
Pia kuhusu zile tuhuma za ubakaji zilizoletwa mbele ya mashabiki wa Timaya na mwanamke aliyefahamika kama Shella B zinaendelea kuharibu maisha ya Timaya baada ya mwanadada huyo kuonyesha ripoti ya polisi inayohusishwa na tukio hilo.Maswali kwa baadhi ya fans wa Timaya>>> Je Timaya ataruhusiwa tena kwenye kufanya show nchini Marekani ?
Mpaka Shella B ametoa wimbo unaozungumzia tukio lote la kubakwa na Timaya.
Picha ya mtoto Grace@via Instagram


Post ya Shella B@via Instagram

Picha | Kcee wa Nigeria akutana na Akon kibiashara zaidi.

Mwimbaji wa Nigeria Kcee anayefahamika kwa hit kama ‘Limpopo’ amepata nafasi ya kukutana na C.E.O Wa Konvict music records na Kon Live Distribution ‘Akon’ alivyokuwa Nigeria katika Project yake ya Light Up Africa mji wa Lagos ambapo alifikia katika hotel ya Eko.Kcee ameonekana akiwa kwenye mazungumzo marefu na Akon yanayosemekana kuwa ni biashara zaidi.



Picha | Timaya wa Nigeria akutana na Rihanna, Rihanna aupenda wimbo wa Bum Bum.


Msanii kutoka Nigeria Timaya ameonekana kwenye visiwa vya Barbados kwenye tamasha la muziki akiwa na Bad girl Rihanna. Timaya  na Rihanna walipiga picha pamoja na baadae Rihanna alionekana akicheza wibo wa Timaya ‘Bum Bum’. Inasemekana kuna collabo inakuja na itafanywa na Don Jazzy.

Video | Yohana Ft Young Killer ‘Uhai wangu



Yohana Ft Young Killer ‘Uhai wangu

Hii video ya Yohana ambayo kafanya kazi na kijana Msodoki toka jiji la Rock City,  Yohana Ft Young Killer ‘Uhai wangu’ Ni kazi ya director Joowezy, Itazame hapa

Kuhusu Dk. Slaa kumkataa Lowassa



UKAWA MOJA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa.
Na Waandishi Wetu
NI kweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo umeibuliwa.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.
ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH!
Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa yupo.”
MTOA HABARI ASHIRIKI VIKAO
“Mimi ninayekwambia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, nimeshiriki zaidi ya vikao 14 vilivyokuwa vikimjadili Lowassa na vyote hivyo, Dk. Slaa alikuwepo. Huyu jamaa hajakaribishwa kwa utashi wa mtu mmoja kama mnavyosikia huko nje na wala mzee Mtei (Edwin, mwasisi wa chama hicho) hahusiki na chochote,” alisema mjumbe huyo.
WABUNGE WAKOROFI WALIAFIKI
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, ili kuondoa dhana kuwa, Lowassa anapelekwa Chadema na uongozi, wabunge wote ‘wakorofi’ ndani ya chama hicho walikaribishwa kushiriki vikao 14 vya kumjadili ili pia wamuulize maswali na yapate majibu kitu ambacho kilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aliwataja baadhi ya wabunge hao ‘wakorofi’ na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Godbless Lema (Arusha Mjini), John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joshua Nassari (Arumeru), Ezekiel Wenje (Nyamagana),  David Silinde (Mbozi Magharibi) na Highness Kiwia (Ilemela).
“Unajua, kwa vyovyote vile, vikao kama vingefanywa na viongozi wa juu peke yao, hawa wabunge wakorofi wangesumbua sana, lakini wote walishiriki na hakuna ambacho hawakijui. Ndiyo maana wote wamekaa kimya kwa sababu taratibu zote zilifuatwa,” alisema mjumbe huyo.
UKWELI ULIVYO
“Hapa lazima nikueleze ukweli. Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea hakina masilahi kwa familia.
YADAIWA DK. SLAA ALITAKIWA KUCHAGUA MOJA
Mjumbe huyo alikwenda mbali kwa kusema kuwa, wakati wa mchakato wa Dk. Slaa kutaka Lowassa aingie Chadema baada ya kukatwa jina na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, hakuiambia familia yake mpaka dakika za mwisho, ikajulikana.
“Ndipo familia ikamweka chini na kumwambia achague moja. Aendelee na siasa za Chadema au aachane  na siasa hizo ili  aangalie familia yake kwani kitendo chake cha kuwa mstari wa mbele kumtaka Lowassa kiliashiria kuwa, yeye hatagombea tena urais hivyo kuua matumaini ya familia. Ndiyo maana yupo kimya na hafiki ofisini.”
CHADEMA YAPANGA SAFU YA KUMSHAWISHI
“Sasa dokta ni mtu mzima. Hawezi kuliamua hilo kirahisi kama unavyofikiria. Ni lazima aende nalo taratibu ili kuziridhisha pande zote mbili. Na kwa kutambua hilo, chama kimeunda jopo la watu, wakiwemo mapadri, mashehe na marafiki zake ili wamshawishi arejee Chadema lakini akiiweka familia yake katika kuridhia na kumwelewa,” alisema mjumbe huyo wa Kamati Kuu.
LOWASSA AANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND
Kuhusu madai ya muda mrefu ya chama hicho yanayomtaja Lowassa kuwa ni fisadi, mjumbe huyo alisema kiongozi huyo aliwaeleza kwa ufasaha kuhusu utajiri wake na wakaridhika. Kwa upande wa Richmond, aliwaeleza kuwa alishataka kuuvunja mkataba huo, lakini mamlaka ya juu ikamzuia.
TAASISI TOKA NJE YATUA NCHINI KUTAFITI
Juu ya nafasi yao kushinda urais wakiwa na Lowassa, mjumbe huyo alisema kabla ya kuafiki kumtangaza kugombea, kwa gharama za Chadema, walikodi taasisi ya utafiti kutoka nchini Ujerumani kuja Tanzania ili kufanya utafiti nchi nzima kama Lowassa anakubalika.
Alisema utafiti ulipokamilika, ikaonesha kuwa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika Julai 2015, Lowassa alikuwa mbele ya wagombea wenzake kwa asilimia 65.
SLAA KIMYAAA!
Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Dk. Slaa hajajitokeza kuelezea kilichosababisha ukimya wake huku akiwa hapokei simu ya Uwazi kitu kinachozidisha kwa kasi maneno mitandaoni juu ya hatima yake ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Alhamisi iliyopita gazeti dada na hili, Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, waandishi wake walishinda nyumbani kwa Dk. Slaa, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar lakini walishindwa kuongea naye licha ya kumpelekea karatasi yenye ujumbe wa kumuomba kuzungumza naye, waliambulia kumuona kwa mbali akiwa ndani ya geti la nyumba yake.

DIAMOND, AUNT WAONGOZA SHANGWE ‘BIRTHDAY’ YA MOSE IYOBO



USIKU wa kuamkia leo dansa wa Crow ya Wasafi Classic Baby, Mose Iyobo, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake iliyohudhuriwa na  baadhi ya mastaa akiwemo bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel, ambapo kwa pamoja waliongoza shangwe kwenye pati hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa hoteli ya Regence iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo mastaa na watu kibao  walihudhuria wakanywa na kukata keki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa sherehe hizo.






Download | D -TWICE School Baby



Download | Young Killer ft Maua-Do for Love



MWANA FA AFUNGUKA SAFARI YAKE YA MUZIKI




Download | Bin Simba ChoZi(Prod Double Y)



Video | Navy Kenzo ft Vanessa-Game>>>>Watch IT




Download | STIMO Baby Girl



Download | One Shaba-Juma Mashughuli




Download | STIMO-MA GIRL




Video mpya ya King chiwah Ft Hasna ‘Lover Lover


Hii video mpya ya msanii aliyewahii kuwa na kundi la TNG King chiwah ‘Lover lover’ Ft Hasna, Bonyeza Play Kuitazama



WEMA AKITONGOZWA NA NUH MZIWANDA




Nay Wa Mitego atoa sababu za kwanini yeye ni role model bora kwa vijana.

Rapa Nay wa Mitego amekuwa miongoni mwa wasanii wasioficha mafanikio yao waliyopata kupitia muziki, hizi ni baadhi ya sababu za kwanini yeye ni Role Model Bora zaidi.

VIDEO

Diamond Atoa Shukrani zake za dhati

Thanks alot to my all Fans around the World, for your unconditional love and Support that you been Giving me... i can't even explain how grateful i am... two awards on NollyWood & African People Choice Awards @Africannafca
FAVOURITE SONG OF THE YEAR (Nana)
FAVOURITE ARTIST OF THE YEAR
thanks alot @Africannafca
(Naomba nitumie Muda huu kuwashkuru Mashabiki zangu wote kwa Mapenzi na Sapoti yenu ya Dhati mnayoendelea kunipa...ningependa niwataarifu kuwa kijana wenu mmeniwezesha kushinda tunzo mbili ambazo ni MSANII ANAEPENDWA AFRICA na NYIMBO INAYOPENDWA AFRICA (#NaNa ) kwenye Tunzo za NollyWood & African people Choice Awards @Africannafca zitazotolewa tarehe 12 /09 /2015



BREAKING NEWS


Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu  mmesimamia wapi katika suala hili.
Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomi, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa.

Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikuwa 'corrupt' swali ni kwanini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuwa mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995. Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe kinamna!


Mimi namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995. Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?


Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo? Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chake cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.


Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!


Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.



LIKE FATHER LIKE SON*REMIX(COMING SOON)

KAENI MKAO WA KULA


A photo posted by NCHI YA AHADI (@kalajeremiah) on

Yemi Alade - Duro Timi


Davido akubali kufanya collabo na Ali Kiba


Davido asema Tanzania ni nchi ya pili kuichukulia kama nyumbani ndio maana alipost bendera ya Tanzania hivi karibuni.
Davido ambaye ameshinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwenye Mtv Afrika Music Awards amemtaja Ali Kiba kama msanii anayefata kwenye orodha ya wasanii atakao fanya nao kazi Tanzania. Matumaini yake ni kazi kwenda vizuri kati yake Davido na Alikiba.

EDU_BOY_FT_BARAKAH DA PRINCE_-_NI_WEWE(DOWNLOAD NEW AUDIO)